Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AHUDHURIA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD SAW ZANZIBAR.

$
0
0



 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulid ya Mfungo Sita Zanzibar  Sheikh Shirali Champsi alipowasili katika viwanja vya  maisara Zanzibar kuhudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).(Picha na Ikulu)
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaaf Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Al Hajj Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali wakiwa wamesimama wakati wakutoa Salamu za kumkaribisha qaswida iliokuwa ikisomwa na Madrasatul E Itiswam ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 /MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Wananchi na Viongozi wakisimama wakati wa kutoa salamu ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj  Ali Mohamed Shein alipowasili katika viwanja hivyo kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) (Picha na Ikulu)
 WANAFUNZI wa Madrasatul E’itiswam ya Chukwani Zanzibar wakisoma Qwasid ya Salamu ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al Hajj, Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya maisra Zanzibar.(Picha na Ikulu
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alhajj Ali Mohamed Shein, alkisoma ratiba ya hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.(Picha na Ikulu)
 KADHI Mkuu wa Zanibar Sheikh Khamis Haji akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya waalikwa katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya waalikwa katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 /USTADH  Hamadan Juma Hamdan kutoka magogoni Mkoa wa Mjini Unguja akisoma Quran surah Fat-h aya ya 4 hadi ya 10, kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.(Picha na Ikulu
 WAUMINI wa Kiislam Zanzibar wakihudhuria kuadhimisha sherehe Tufuku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj Ali Mohamed Shein, akijumuika katika sherehe tukufu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WANAFUNZI wa Madrasatul Insania kutoka roundabout magogoni Mkoa wa Mjini Unguja wakisoma Qaswida ya Yarabbi Swalli wakati wa hafla hiyo ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume (S.A.W)Zyaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 USTADH Juma Fakhi Omar kutoka Amaan Mkoa wa Mjini Unguja akisoma mlango wa  kwanza wa Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika Kitaifa katika viwanja vya Maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi na Viongozi wa Serikali katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)

 VIONGOZI wa Serikali na Dini Zanzibar wakihudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara wakiwa wamesimama wakati Qiyam Taala. Ikisomwa Qaswida na Madrasatul Qamaria ya kibanda hatari Zanzibar.(Picha na Ikulu)




 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na Wananchi wakiwa wamesimama Qiyam Taala wakati wa hafla hiyo ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles