Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, (kulia), akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na watumishi na viongozi wa Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam Januari 5, 2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe “amekunjua makucha.” Baada ya kutangaza kumsimamisha kazi mara moja kuanzia Januari 5, 2016 Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima kupisha uchunguzi wa upotevu wa mapato ya Serikali tangu mwaka 2012 hadi sasa.
Hatua hiyo ya Profesa Maghembe, imeelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa ni kwenda sambambana kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na hivyo kufuta maneno yaliyokuwa yakitolewa hapo nyuma wakati waziri huyo akiwa waziri kwenye serikali ya awamu ya tano na kuitwa kuwa ni miongonimwa mawaziri “mizigo”.
Waziri pia ametoa siku saba (7), kwa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kutumia muda kurudi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama Mpingo House na kutoka huko walikopanga jingo la NSSF Mafao House lililopo Ilala. “Naagiza jumatatu Januari 11 nikipita pale gorofa ya tatu ya jingo hili, nikute mmesharudina mnachapa kazi.” Alisisitiza Waziri Maghembe ambaye alijkuwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
Waziri alitoa maagizo hayo Januari 5, 2016 wakati baada ya mkutano wake na maafisa wa wizara hiyo uliofanyika jingo la “Mpingo” ambalondio makao makuu yake jijini Dar es Salaam
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari, Prof. Maghembe amesema agizo la kumsimamisha kazi kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima ni kutokanana ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Pia ameagiza maofisa hao wote wanaokusanya maduhuli ya Serikali katika Wilaya watumie muda wa siku kumi kuanzia Januari 5, 2016 kuhakikisha vitabu vyote vyenye taarifa za maduhuli vinawasilishwa kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kuyakagua.
“Ndugu naibuKatibu Mkuu, tunaomba utusaidie kwa hili, wasliana na ofisi ya Mkaguzina Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ili vitabu hivi vikaguliwe mara moja.” Aliagiza.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na watumishi wa Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam Januari 5, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.(Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, (wapili kulia), akizungumza kwenyemkutano huo
Afisa MtendajiMkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS), Bw. Juma Mgoo (kulia), akiwasilisha taarifa ya ofisi yake
Baadhi ya waliohudhuria mkutano huo
Profesa Maghembe (katikati-mbele, akizungumza na watumishi hao
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Bi. Gladnes Mkamba (kulia aliyesimama, akiwasilisha taarifa ya idara yake