Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Ibrahim Class awapa Watanzania kile walichotarajia

$
0
0
 Bondia  Mtanzania Ibrahim Class (kushoto) akipambana na na Mwenzie kutoka Afrika Kusini  Koos Sibiya katika pambano la kimataifa la ngumi lenye mizunguko  kumi na mbil lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambalo mtanzania huyo alishinda.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza  Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa  lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
P Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliojitokeza katika pambano la ngumi la kimataifa kati ya mtanzania Ibrahim Class pamoja na Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.

 .Mabondia wanawake Felicha Mashauri (mwenye kaptula nyekundu) dhidi ya Happy Daudi wakizipiga jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa  kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.
Bondia Haidari Mchanjo akifurahia ushindi wa mizunguko sita alioupata dhidi ya Bondia Bakari Magona  lililochezwa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa  kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles