AZIRI MKUU AONGOZA KUZINDUA DUKA LA BOHARI YA DAWA (MSD), MPANDA, MKOANI KATAVI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Dawa la Bohari ya Dawa (MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Katavi, Peter Mselemu, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Jiwe la Msingi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu wakifurahi wakiwa ndani ya duka hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa MSD.
Mwonekano wa duka hilo la MSD, mkoani Katavi.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema utaratibu wa MSD wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji litaboresha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za kununua dawa kutoka nje ya nchi.
Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la dawa la MSD, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, ambalo linaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka 7 ya dawa nchini.
Waziri Mkuu pia amesema kwa mwaka huu wa fedha shilingi Bilioni 251 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ili kupunguza changamoto za uhaba wa dawa na kueleza kuwa shabaha ya serikali ni kufikia asilimia 95-100 ya upatikanaji wa dawa hadi itakapofika mwezi Juni, 2017.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa duka hilo wataliendesha kwa mwaka mmoja tu,na kisha kulikabidhi kwa Halmashauri ili iliendeshe na kuongeza mapatao yao.
Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Bwanakunu amesema kuwa kwa sasa fedha sio tatizo,na dawa zinaendelea kuagizwa kulingana na mahitaji.