Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la Mapinduzi nahodha wa Timy ya Azam John Bocco 'Adebayor' baada ya kuwafunga timu ya Simba goli 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika hivi usiku uwanja wa Amaan Zanzibar
Wachezaji wa timu ya Azam wakinyanyua juu kombe la ubingwa wa michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kuwafunga Simba 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika hivi usiku uwanja wa Amaan Zanzibar
Wachezaji wa Timu ya Azam wakishangiria mbele ya mwari wao Kombe la Mapinduzi Wachezaji wa Timu ya Azam wakimtembeza mwari wao baada ya ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Simba
Wapenzi wa Timu ya Azam wakiwapa hongera wachezaji wa timu hiyo baada ya ushindi na kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi 2017