Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kulia), akipeana mikono na Katibu Tawala Msaidizi (anayeshughulikia masuala ya serikali za mitaa), jijini Dar es Salaam, Bi. Merry Assey, baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika Januari 3, 2017 kwenye makao makuu ya PSPF Golden Jubilee Towers jijini.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umeendesha semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwajengea uwezo wa kushughulikia matatizo ya wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo.
Mafunzo hayo ya siku mbili, yameanza leo Januari 3, 2017, na kufunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi (sehemu ya serikali za mitaa), Bi. Merry Assey kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ea Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Niipongeze PSPF kwa kuandaa semina hii ambayo inatoa fursa ya watumishi hawa waliohudhuria katika mafunzo haya kuelewa huduma na shughuli zinazofanywa na Mfuko huu na kwa maana hiyo iwe rahisi kwenu kutatua kero za wananchi wanaofika pale Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta ufumbuzi hususan kwa wanachama wa Mfuko huu,.” Alisema Bi. Assey, wakati akifungua semina hiyo.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, alisema, PSPF ilifikia uamuzi wa kuandaa semina hiyo kufuatia wazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye alitaka kujengewa uwezo kwa watumishi wa Ofisi yake ili waweze kuwahudumia vema wananchi wakiwemo wanachama wa PSPF.
“Nililipokea wazo hilo na sisi PSPF tukaona ni fursa nzuri kwa kuwaelimisha watumishi hawa ambao, ninahakika baada ya mafunzo haya, watakuwa mabalozi wetu wazuri lakini pia na wao watajiunga na Mfuko huu.” Alisema Bw. Mayingu.
Mada mbalimbali zilitolewa kwa wanasemina hao ikiwa ni pamoja na ile ya shughuli za Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko huo, Bi. Neema Muro, Kaimu Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi na Maafisa wengine wa Mfujko huo.
Bi. Merry Assey, akifungua semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini
Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza wakati wa semina hiyo
Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Neema Muro akitoa mada juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Pensehni wa PSPF
Kaimu Meneja Mafao wa PSPF, Bw.Haji Moshi, akitoa mada ya namna mwanachama wa Mfuko huo anavyoweza kupata mafao yake
Bw. Haji Moshi akitoa mada
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitoelwa na viongozi na maafisa wa PSPF
Baadhi ya washiriki wakipitia vijarida vyenye maelezo ya kina kuhusu huduma zitolewazo na PSPF
Mshiriki akisoma kijarida cha PSPF
Mkurugenzi wa Huduma wa PSPF, Bi. Neema Muro, (wapili kulia), akiongozana na Mameneja na maafisa wa Mfuko huo wakati wakielekea chumba cha semina kutoa mafunzo kuhusu huduma za Mfuko
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa PSPF na Ofisi ya RAS, Dar es Salaam
Picha ya pamoja
Baadhi ya mameneja wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja na "meza kuu"