Na K-Vis Media/Khalfan Said
HATIMAYE kitendawili kimeteguliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 10, 2015 ametangaza baraza la Mawaziri litakaloundwa na wizara 18 tu.
Akitangaza baraza hilo huku akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Rais Magufuli alianza kwa kusema, “Walioteuliwa wasifikirie kufanya sherehe kwa sababu kazi niliyowapa ni ngumu, ila wajiandae kufanya sherehe wakifukuzwa.” Alisema.
Rais amesema, hakutakuwa na semina elekezi na kwamba fedha zilizotengwa shilingi Bilioni mbili, kwa ajili ya semina hiyo, zitaelekezwa kwenye shughuli nyingine za kijamii kama elimu. “ Watajipa semina wenyewe humo humo ndani” alisisitiza.
Baraza hilo jipya la serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kama ifuatavyo, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, kutakuwa na mawaziri wawili ambao ni George Simbachawene na Angellha Kairuki, Naibu waziri atakuwa Jaffo Selemani Said, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na mazingira, Waziri atakuwa Januari Makamba,na Naibu waziri Luhaga Mpina, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama, naibu waziri, Dkt. Possi Abdallah, naibu waziri mwingine ni Anthony Mavunde, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchema, Naibu Waziri William Ole Nasha, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri (bado), naibu waziri, Injiania Armandus Ngonyani, Wizara ya Fedha na Mipango, (bado), naibu waziri ni Dkt.Ashantu Kijaji, Wizara ya Nishati na Madini, Waziri ni Profesa Sospter Muhongo, naibu Waziri ni Dkt.Medard Karemagi, Wizara ya Katiba na Sheria, Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Masharioki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga, kuwa Mbunge na ameteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo, Naibu waziri ni Dkt. Suzan Alfions Kolimba, Wizara ya Ulinzi na Jeshio la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri ni Bw. William Lukuvi, Naibu wake ni Bi. Angelina Mabula, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Naibu wake, ni Injinia Isack Kamwela, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee, Waziri ni Bi. Ummy Mwalimu na Naibu wake ni Dkt. Khamisi Kigwangala, Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Waziri ni Bw. Nape Nnauye na Naibu wake ni Bi. Anastazia James Wambura, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Elimu, (Waziri bado), naibu wake ni Injinia Stella Manyanya, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri ni Bw. Charles Mwijage, Wizara ya Maliasili na Utalii, (Waziri bado), Naibu wake ni Injinia Ramo Makani, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga,
Balozi Augustine Mhiga
Dkt. Harrison Mwakyembe
Bw. George Simbachawene
Bi. Angellah Kairuki
Bw. January Makamba
Bw. Nape Nanuye
Profesa Sospeter Muhongo
Dkt. Hussein Mwinyi
Bw. William Lukuvi
Bi. Ummy Mwalimu
Bw. Mwigulu Nchemba