Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
↧