Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli, amemtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika holeti ya Serena Jijini Dar es Salaam. Maalim Seif yupo hotelini hapo kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitali ya Hindu Mandal jana jioni alipokuwa amelazwa.
Maalim Seif amewahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida. (Picha na Salmin Said, OMKR)