Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Article 0

$
0
0

IMG_9916IMG_9920
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania.
Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.
Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.
Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.
"Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.
Aidha Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi ya aina mbalimbali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles