Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Article 7

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri (wapili kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (watatu kushoto) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho jijini Dares Salaam, leo Desemba 31, 2015. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo)
 Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa  ziara ya kikazi ya Mhe. Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.

Na Aron Msigwa MAELEZO.

Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali  kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.

Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua  pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu  Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.

Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za  umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.

Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa Ameeleza Mhe. Angella.

Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango  wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini  kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo.

Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao  ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA.
Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya  ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida.

katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha


Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo  mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov)  kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma.

Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote  ziweze kupatikana katika eneo moja  na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.

Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.

Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa.


 



Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojiana Elimu ya Juu, Profesa Joyce Ndalichako, ameaapa kula sahani moja na wamiliki wa shule za sekondari na msongi za watu binafsi kuongeza ada lakini mbaya zaidi kuongeza "cha juu", yaani michango ya maendeleo na majengo. "Hivi uliombaje usajili wa shule wakati huna majengo, sitaki kusikia hii kitu inaitwa michango ya majengo au maendeleo" kwenye shule za binafsi na hili nitalifanyia kazi mimi binafsi." aliapa Profesa Ndalichako muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa wa Uwaziri wa Elimu, Sayansi, Teknolijia na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Profesa Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Braza la Taifa la Mitihani, alisema, shule zote zinaziomilikiwa na serikali hazitatoza ada wala michango ya aina yoyote kwa wanafunzi wa kuanzia shule za awali hadi kidato cha nne kuanzia mwaka wa masomo 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Progesa Joyce Ndalichako

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Coat of arms of Tanzania.png

KATAZO LA KUONGEZA ADA KWA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2016
Waraka wa Elimu Na. 4 wa Mwaka 2008 uliweka viwango vya ada vinavyotozwa katika shule za Msingi na Sekondari za Serikali na zile zisizo za serikali. Ada iliyowekwa kwa shule za kutwa zisizo za serikali ni Tsh. 150,000/= na shule za bweni Tsh. 380,000/= kwa mwaka kwa kila mwanafunzi. Aidha waraka huo ulielekeza kwamba ongezeko lolote la ada lazima lipate kibali cha Kamishna wa Elimu kabla ya kuanza kutumika.  
Hata hivyo imegundulika kuna baadhi ya shule zisizo za serikali zimekuwa zikiongeza ada kila mwaka pasipo kupata kibali cha Kamishna wa Elimu. Utamaduni huu wa kuongeza ada kila ifikapo mwishoni mwa mwaka umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa kwa wazazi/walezi na hata baadhi yao kushindwa kuendelea kusomesha vijana wao katika baadhi ya shule.
Kwa tangazo hili wamiliki wote wa shule zisizo za serikali wanaagizwa kufanya yafuatayo:
1.      Kutokuongeza gharama za uendeshaji wa shule zikiwemo ada kwa mwaka wa masomo unaoanzia mwezi Januari mwaka 2016 mpaka watakapopata maelekezo kutoka kwa Kamishna wa Elimu; wale ambao tayari wameongeza gharama na ada kwa mwaka wa masomo wa 2016 bila kibali cha Kamishna wa Elimu, Wizara haitambui ongezeko hilo kwa kuwa ni batili na hivyo zimefutwa.
2.      Ada zote kwa shule zisizo za serikali zitabaki kama zilivyokuwa zimeidhinishwa na Kamishna wa Elimu.
3.      Kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Shule aliyepo Idara ya Ithibati ya Shule inayoeleza kiasi cha ada na gharama kinachotozwa kwa sasa (kabla ya mwaka wa masomo 2016) na tarehe shule ilipopata kibali kutoka kwa Kamishna wa Elimu kutoza kiwango hicho cha ada.  Taarifa hiyo ifike ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe ya tangazo hili.
Wathibiti ubora wa shule waliopo sehemu mbalimbali nchini wanaagizwa kulifuatilia suala hili kwa karibu ili kila shule itekeleze agizo hili na kutoa taarifa zilizoelekezwa katika tangazo hili. Hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa wamiliki ambao hawatatekeleza maagizo haya.  
Aidha Wizara iko katika hatua za mwisho za utafiti na kuandaa mfumo wa kielektroniki wa kutambua gharama za kumsomesha mwanafunzi katika elimumsingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na hivyo wadau mbalimbali watoe ushirikiano kwa timu za wataalamu wanaofanya kazi hii ili kusaidia katika kuukamilisha mfumo na hatimaye kuwa na ada elekezi kat







Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles