Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi, akishikana mikono na mlezi wa watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati akikabidhi msaada wa magodoro 20 ambapo pia walilipia bima za afya ya NHIF kwa watoto wote 46 wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), wakibeba moja ya magodoro 20 waliyopewa msaada na Kampuni ya Tanga Cement katika hafla ambayo pia kampuni hiyo ililipa bima za afya ya NHIF kwa watoto wote 46 wa kituo hicho kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana. Katikati kushoto ni mlezi wa kituo, Sista Irene Kafuka na Meneja Rasilimali Watu wa Tanga Cement, Diana Malambugi.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Nancy Mkoyogo (kulia) akishikana mikono na mlezi wa watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati wakikabidhi msaada wa magodoro 20 pamoja na kulipia bima za afya ya NHIF kwa watoto 46 wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kulia), akigawa chakula kwa watoto kituoni hapo jana katika hafla hiyo.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), huku mlezi wa watoto kituoni hapo Sista Irene Kafuka (kulia), akiangalia.
Mmoja wa wafanyakazi wa Tanga Cement, Changwa Mjella, akisaidia kumlisha chakula mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakati wa tukio hilo.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), wakibeba moja ya magodoro 20 waliyopewa msaada na Kampuni ya Tanga Cement katika hafla ambayo pia kampuni hiyo ililipa bima za afya ya NHIF kwa watoto wote 46 wa kituo hicho kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana. Katikati kushoto ni mlezi wa kituo, Sista Irene Kafuka na Meneja Rasilimali Watu wa Tanga Cement, Diana Malambugi.
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kulia), akigawa chakula kwa watoto kituoni hapo jana katika hafla hiyo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho akionyesha umahiri wake wa kusakata muziki wa kizazi kipya katika hafla hiyo. (Picha zote na Mgongos Photography) |