Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Article 4

$
0
0


LIGI KUU ENGLAND, ARSENAL YATAKATA NYUMBANI NA KUONGOZA LIGI KWA MUDA, WATFORD WALIZWA NA TOTTENHAM

Katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini England zilizochezwa jana usiku, washika bunduki wa jiji la London Arsenal waliendeleza ubora wao dimbani baada ya kuitandika Bournemouth mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Emirates. 

Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na wachezaji Gabriel katika dakika ya 27, huku Mesut Ozil akiifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 63. 

Kwa matokeo hayo, Arsenal ndiyo inayoongoza ligi wakiwa na pointi 39.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu England uliochezwa hiyo jana, Watford wakicheza nyumbani walikubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Tottenham Hotspur. 

Katika mchezo huo, Watford walijikuta pungufu uwanjani baada ya Nathan Ake kupewa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya mchezaji wa Tottenham.
 Mwamuzi wa mchezo huo, akimzawadia kadi nyekundu Nathan Ake ( jezi namba 16 ) 
Nao Everton wakiwa nyumbani kwao walipata kipigo cha mabao 4-3 toka kwa Stoke. Mabao ya wenyeji Everton yalifungwa na Lukaku katika dakika ya 22 na 64, Deulofeu akifunga bao jingine katika dakika ya 71. 

Mabao ya Stoke yalifungwa na Shaqiri aliyepachika wavuni mabao mawili katika dakika za 16 na 45, bao la tatu lilifungwa na Joselu kunako dakika ya 80 na bao la nne lilifungwa naArnautovic katika dakika ya 91.
Norwich waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 toka kwa wageni wao Aston Villa. 
Kizaa zaa kingine cha ligi kuu nchini England usiku wa jana kilikuwa ni kati ya West Brom dhidi ya Newcastle. Mchezo huo ulimalizika kwa wenyeji West Brom kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0, goli lililofungwa na nahodha wake Darren Fletcher kwa kichwa saafi kama anavyoonekana pichani juu.
Nao Crystal Palace wakicheza nyumbani walijikuta wakigawana pointi na Swansea baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana bao.








Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles