Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndg. Kheri James baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Maguful Akifungua mkutano wa jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Balozi Job Lusinde baada ya Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana akiwa na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
PICHA NA IKULU
w21: Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Generali John Julius Mbungo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w22: Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.