Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimfariji Ndg. Esther Gama mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Christina Mndeme (kulia) baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Ruvuma tayari kuelekea katika mazishi ya aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama yanayofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.