

Inatajwa kuwa mama huyo Bi. Zulfa ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 48, alifariki hapohapo baada kuangukiwa na mti huo, ambapo licha ya mvua hiyo ya upepo kusababisha kifo pia inatajwa kuezua mabati ya baadhi ya nyumba eneo hilo la kata ya Viwege Bomba Mbili.

DC Mjema ametembelea eneo hilo na kutoa pole kwa familia na kuwaambia kuwa serikali ipo pamoja nao.


Katika hatua nyingine DC Mjema ametembelea Shule ya Msingi Kigogo Fresh ambayo wiki mbili zilizopita ilikubwa na maafa ya mvua kuathiri miundombinu ya shule hiyo na kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi kukosa madarasa ya kukalia hali iliyopelekea shule kufungwa.

Siku ya leo DC Mjema ametembelea shule na kushuhudia ukarabati na ujenzi wa madarasa manne yakiwa yamekamilika jambo ambalo litapelekea zaidi ya wanafunzi 500 kusoma kwenye madarasa hayo.

Ambapo pia DC Mjema ameagiza ujenzi wa madarasa mengine mawili ambayo ameahidi yatakamilika ndani ya miezi miwili na kuleta tumaini jipya kwa wanafunzi hao, halikadhalika ujenzi wa daraja na barabara jambo litakalo saidia wanafunzi na wakazi wa eneo hilo kuvuka bila ya kuwa na wasiwasi.