Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Kagera ikiwa na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya. Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari 19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho.
Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017.