Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein akikata Utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Desemba 30, 2016. Wanaoshuhudia ni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto). (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)
Rais akifunua kitambaa kuzindua msikiti huo
Rais, akipokelewa wakati akiwasili kwenye ufunguzi huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakati alipowasili katika ufunguzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo Desemba 30, 2016. Msikiti huo umejengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa Kampuni ya Al-Buwardy Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw.Samir Ayoub mmoja wa wanafamilia ya Yakoub Othman, msimamizi wa ujenzi wa msikiti huo.
Sheikh Otman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa Msikiti Masjid Muhammad (S.A.W)
Rais akihutubia waumini baada ya ufunguzi huo
Waumini waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa msikiti huo
Ni wakati wa sala