Na Peter Mwenda
WAREMBO 15 wanaingia kilingeni kumtafuta mrembo wa Chang/ombe Miss Chang'ombe katika mashindano yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa yatakayofanyika ukumbi wa TCC Sigara.
Mratibu wa Mashindano hayo, Gervas Sinkala alisema jana kuwa maandalizi wa mashindano hayo yamekamilika na warembo wote wamejiandaa vya kutosha kuwani taji hilo.
Alisema mrembo watakaowania taji hilo ni Anita Medard, Prisca Sarakikya, Diana Joseph, Leah Hamad, Zuhura mohamed,Shani Mshamu, Hadija Masoud, Zahara Msangi na Devotha Benard.
Wengine ni Nancy Mushi, Irene Bega, Sharifa Said, Jesca Nassari, na Sabrina Ramadhani ambao washindi watatu wa kwanza watazawadiwa zawadi nono na kupewa nafasi ya kusoma kozi katika chuo cha DATASTAR Training .
Alisaema mashindano hayo yatafuatiwa na burudani ya muziki kutoka katika bendi ambayo alisema itatambulkishwa kumbini hapo