Katibu mkuu wa TAMISEMI, Musa Iyombe akishikana mkono na Fakri Karim, Meneja Program kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) mara baada ya kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi
Serikali ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) na mashirika mawili yasiyokuwa ya kiserikali ambayo ni Haki Kazi catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) wamezindua mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi wazinduliwa.
Mradi huo kwa mara ya kwanza ulianza kwa majaribio kati ya mwaka 2012 hadi 2013 katika Halmashauri tatu (3) za wilaya za Longido, Ngorongoro, na Monduli Mkoani Arusha.
Baada ya awamu hiyo ya majaribio kumalizika na kuonesha mafanikio makubwa mradi huo umerejea tena awamu hii ukihusisha Halmashauri nyingine 12 katika mikoa ya Manyara, Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Lindi na Dodoma na utasimamiwa na TAMISEMI kwa msaada wa kiufundi na rasilimali fedha kutoka kwa serikali ya Uingereza (UK-AID) na Mfuko wa Umoja Wa mataifa wa maendeleo (UNCDF).
Mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2021) ambapo awamu ya kwanza itaanza kutekelezwa kuanzia mwaka huu 2016-2018 na awamu ya pili ikianza mwaka 2018-2021.
Kupitia mradi huo unalenga kuijengea uwezo Ofisi ya Raisi –TAMISEMI katika maene makubwa mawili ambayo ni uimarishaji wa taasisi katika uratibu wa mradi na uwezo wa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ziweze kutoa elimu kwa jamii kutambua na kutekeleza Miradi ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.
Katibu mkuu wa TAMISEMI, Musa Iyombe aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Goerge Simbachawene katika uzinduzi huo, anasema kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi sasa ni tatizo kubwa na tayari yamelta madhara makubwa katika maisha ya binadamu na pia katika uchumi wa taifa na kuleta mzigo mkubwa kwa taifa la Tanzania.

Kunizio Manyika, Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo

Lucy Ssendi, Mkurugenzi Msaidizi, TAMISEMI, akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa uzinduzi wa mradi huo

Alais Morindat, Mwakilishi Msahuri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), (IIED) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo

Picha ya Pamoja