Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.Watu wanane waliuawa kwa kuchinjwa na watu hao wasiojulikana mapema wiki hii kwenye kijiji hicho. Naibu waziri huyo ambaye alifuatana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Ernest Mangu, pia waliwatembelea wafiwa na kuwapa pole ambapo Naibu waziri ameapa Serikali kuwasaka watu hao na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Naibu waziri Masauni akitembelea eneo hilo "hatari"
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akizungumza katika Kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigella. Watatu kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (wapili kushoto). Viongozi hao wamekutana mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale