Wasani wa Katoro Geita wakicheza ngoma ya Kisukuma wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo Machi 17, 2016., Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waizri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mtambo wa kukamu mafuta ya alzeti wanaushishirika wa Chato akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita Machi 17, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika huo Elias Kaswahili(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro , Geita Machi 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MISS Tanzania, Lilian Kamazima, akitoka kwenye mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2016. Uzinduzi rasmi wa msimu wa mashindano makubwa kabisa ya urembo hapa nchini, Miss Tanzania 2016, yatazinduliwa Jumamosi Machi 19, 2016 kwenye hoteli ya Ramada iliyoko Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, amewaambia waandishi wa habari
Miss Tanzania, Lilian Kamazima, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Hashim Lundenga, akiwa na Miss Tanzania Lilian Kamazima, wakati akiongea na waandishi wa habari Machi 17, 2016
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MSIMU mpya wa amshindano ya ulimbwende, yaani (urembo), ya Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2016, utazinduliwa rasmi Jumamosi Machi 19, 2016 kwenye Hoteli ya Ramada Resort iliyoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo nchini wakiwemo wabunifu wa mabvazi, mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini watakwepo.
Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Lino International, ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo Machi 17, 2016, alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.
Burudani zitakuwepo kama kawaida kunogesha tukio hilo la aina yake ambapo wasanii kama vile Lina na Wanne Star watakuwepo.
Lundenga ambaye alifuatana na Miss Tanzania wa sasa, Lilian Kamazima, na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania, alsiema, mara tu baada ya uzinduzi huo, tukio linguine kama hilo litafanyika jijini Arusha.
Pia mawakala watapatiwa semina ambayo itapangwa baada ya tukio hilo na kasha mashindano ya urembo kwa ngazi za vituo, wilaya, mikoa na kanda yatafanyika.
Makampuni kadhaa yamejitokeza kudhamini mashindano hayo ambapo Lundenga ameyataja kuwa ni pamoja na Ramada Resorts Dar es Salaam, Naf Beach Hotel Mtwara, Kitwe General Trader, CXC Africa, Mwandago Investment Limited, Break Point na GSM Media
Lilian akitaniana na mmiliki wa blog ya Father Kidevu, Mroki Mroki
Lundenga(katikati), Lilian, (kushoto) na Bosco Majaliwa, Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania
Daktari Bingwa wa afya ya kinywa na meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mapema leo asubuhi alipokuwa akiwapa Elimu ya upigaji mswaki na utunzaji wa kinywa kwa ujumla na utunzaji wa miswaki yao mara wamalizapo kupiga mswaki na kuwaomba japo kupiga marambili kwa siku (POCHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Daktari Bingwa wa afya ya kinywa na meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle, akiwatolea mfano kwa Mmoja wa watoto hao
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Germana Vincent akigawa flana kwa mtoto mwenye ulemavu wa macho wanao lelewa katika kituo cha Buhangija
Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanao lelewa katika kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga wakiimba nyimbo ya kuwaombea Dua Madaktari hao wakiwa wameinua mikono yao juu
Baadhi ya Timu ya wasaidizi wa Kituo hicho cha watoto wenye ulemavu wa ngozi akiwemo Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle, (wa pili kulia)
Kiongozi wa Msafara ambaye pia ni Daktari wa Afya ya kinywa na meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Arnold Mtenga (katikati) akiteta jambo na madaktari wenzake, kulia ni Conrad Mselle na kushoto ni Germana Vincent, wote kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili
Muonekano katika picha
Daktari wa wa Afya ya kinywa na meno, Sr. Benjamina Buya (kulia) wa Hospitali ya Huruma DDH yaWilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro akitoa elimu ya Afya ya kinywa na meno kwa walezi na wasimamizi wa kituo hicho
Profesa Lembariti akimwelekeza mwanafunzi wa kituo hicho cha Buhangija kwa matumizi ya mswaki na kutunza Afya ya Kinywa na Meno huku wanafunzi wengine wakiangalia kwa makini
Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja kwenye chumba cha Ofisi ya Hospitali hiyo na madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kulia ni Mmiliki wa ujijirahaa blog, Kamisi Mussa
Profesa Lembariti akizungumza na Mtoto Suzy Aseng (8), wa Shule ya Rittle Treasures ya Bungayambelele Darasa la 4, alipokuja katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mara aliposikia kuwa kunamadaktari wa Afya ya Kinywa na Mane watakua wakitoa huduma ya Afya ya Kinywa na Meno na ndipo alipompa Elimu ya kuhusiana na upigaji mswaki na kumuelekeza mara akiona mswaki unaanza kupinda amwambie mlezi ambadilishie mswaki
Daktari Wa Fya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Germana Vincent (kushoto) akizungumza jambo na Madaktari wenzake wakati walipotembelea Kituo cha Watoto wenye ulemavy wa ngozi wa Kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa Wiki ya Afya na Kinywa na Meno ambapo kilele cha Maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa Mkoani Morogoro Machi 20, 2016, kuanzia kulia ni Dr, Gustav Rwekaza wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya na Dr, Gerald George wa Hospitali ya Jiji la Tanga
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni Dr. Iddi Khery akimuhudumia Mmoja wa Mwanafunzi wa kituo cha Buhangij
Wananchi wa Kalebezo wilayani Chato wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, KassimMajaliwa alipopita kijijini kwao akitoka Ngara kuelekea Chato mkoani Geita machi 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA Mwandishi wetu, CHATO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Bw. Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana usiku (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mshikamano SACCOS wilayani humo.
Afisa Kilimo na Ushirika anadaiwa kuchangisha kiasi cha sh. milioni 20 kutoka kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kuanzisha SACCOS tangu mwaka 2013 lakini hadi sasa SACCOS haijaanzishwa na wala fedha hizo hazijarejeshwa. Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na watumishi watatu (majina yamehifadhiwa). Aidha, Bw. Waryuba anadaiwa kutumia lugha chafu na za vitisho kwa watumishi walio chini yake ikiwa ni pamoja na kuomba na kupokea rushwa, na kunyanyasa na kudhalilisha kijinsia baadhi ya watumishi wa kike.
Inadaiwa pia Bw. Waryuba alikopa bila kufuata taratibu za mikopo wilayani Chato ambapo alikopa sh. milioni 15 kutoka Mwambao SACCOS na sh. milioni 15 nyingine kutoka Chato Teachers’ SACCOS tangu mwaka 2015 na tangu wakati huo hajazirejesha hali ambayo imeleta manung’uniko kutoka kwa viongozi na wananchama wa SACCOS husika.
“Malalamiko ya watumishi na wananchi dhidi ya huyu bwana yamefikishwa kwa Kaimu Mkurugenzi
Afisa Ardhi wa Wilaya ya Ngara, Betty Munuo wa Pili kushoto na Mwenyekiti wa kijiji cha Rwakalaman, Brighton Kemkimba (kulia) wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozunguma katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara machi16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)8252
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Jafari baada ya kuwahutubia wananchi wa kata ya Kasulo wilayani Ngara Machi 16, 2016. Alikuwa katika siku ya mwisho ya zira ya mkoa wa Kagera. (Picha na Ofis ya Waziri Mkuu)