Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Article 7

$
0
0
MWANAMITINDO WA KIMATAIFA MIRIAM ODEMBA KUWA JAJI MAALUM

Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado 
yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji 
maalum katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe 
Tanzania 2015. Majaji wengine watakaoshiriki katika kumtafuta mnyange 
wa mwaka huu ni Sheria Ngowi, Maria Sarungi Tsehai, Mariam Ndaba na 
Priyal wa sia couture.

Zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo 
watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla 
ya fainali tarehe 20 mwezi huu.

Warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa 
waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar 
es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam), 
Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy 
Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody 
Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya), 
Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).

  Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti 
ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.


  Miss Universe PR Department.
  *Compass Communications*



Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles