ABIRIA WA NDEGE ATOSWA ANGANI, NI BAADAYA MWILI WAKE KUSHIKA MOTO
![]()
Tundu lililosababishwa na mlipuko huo na ambalondilolilitumika kumtosa abiria huyo
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said na Mashirika ya Habari ABIRIA wa ndege ashika moto na kutoswa hewani ndege ikiwa angani umbali wa futi elfu 14,000. Kwa mujibu wa abiria mmoja wa ndege hiyo aina ya Airbus 321 Daalo Airlines mruko namba D3159 iliyokuwa ikitoka mjini Mogadishu Somalia, kwenda Djibuti, alitoswa kupitia tundu kubwa upande wa nyuma wa ndege lililotokana na kitu kinachosadikiwa kuwa ni mlipuko. “Nilimuona abiria mwenye umri kama miaka 60 hivi, akitoswa nje ya ndege, palikuwa na kishindo kikubwa, na shimo kubwa likatokea upande mmojawa ndege na mzee huyo akapotea kupitia tundu hilo.”Alisema abiria huyo Hassan Mohammed Nur. “Dakina moja kabla mzee huyo alikuwa ameketikwenye kiti chake, baadaye akapotea.” Alisema. Nur aliripotiwa akisema, mtu huyo alishika moto kabla ya kutoswa kupitia tundu hilo na mwili wa mtu aliyechomeka ulikutwa kwenye mji wa Balad, kiasi cha maili 18 kutoka Mogadishu na hakuna uthibitisho wowote kuwa mwili huo ni wa mtu aliyetoswa hewani kutoka ndani ya ndege. Ndege hiyo Airbus 321 ikiwa na abiria 74 iliruka kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu ikiwa njaini kuelekea Djibuti, dakika 5 tu baada ya kuruka, kishindo cha mlipuko kilisikika na kupelekea shimo lenye upana wa kipenyo cha futi 6 kwa 3, hata hivyo chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana. Rubani wa ndege hiyo alikaririwa akisema, “Nadhani ilikuwa bomu, bahati ni kwamba kidhibiti ndege hakikuathiriwa ndio maana nilifanikiwa kurudi na kutua salama. Abiria mwingine raia wa Ufini, ameripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo lakini hali yake inaendelea vizuri. Soma Zaidi