Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo, lililokuwa safarini likitokea Njombe kuelekea jijini Dar es Salaam, limepeta ajali mapema leo eneo la Kingembasi wilayani Mufindi mkoani Iringa Januari 4, 2016 baada ya kujigonga kwa nyuma kwenye lori lililokuwa limeegeshwa kama ambavyo picha hii inavyoonyesha. Kamanda wa polisi wa mkoa wa mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili, na majeruhi 20, na kwamba uchunguzi wa polisi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo
↧