Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Balozi Dkt. Abdallah Saleh Possi awasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican

$
0
0
Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
 Balozi Dkt. Possi katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Wengine ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdul Mhinte, na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana.

Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu PaPa Francis
Balozi Dkt. Possi akikabidhi hati za utambulisho kama Balozi wa Tanzania Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis.

Balozi wa Tanzania Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. Pamoja na Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.
Kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatikani, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.
Mabalozi wengine waliowasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi Retšelisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,  na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia. 
Baada ya uwasilishaji hati, pia Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuia ya Watanzania wa Vatican. Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles