Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia vicent Mbilinyi kwa kumuelekeza kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcat' Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake na Hussein Shemdoe utakaofanyika katika ukumbi wa musoma Bar siku ya Mei Mosi Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi ya kumkabili Hussein Shemdoe wakati wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi siku ya sikukuu ya wafanyaklazi Dunian mpambano uho utafanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Mwembe Yanga mpambano wa raundi 8
Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa nje ya ulingo kwa mda wa mwaka mzima sasa tangu mwishoni mwa mwaka 2016 na sasa anakuja kivingine
mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia mbali mbali ambapo bondia Shafii Ramadhani atapambana na Antony Mathias wakati Nassibu Ramadhani atavaana na Hamisi Mohamedi na Shomari Galibu atapambana na Hashimu Sheni wakati Said Mlugulu atavaana na Said Bakari 'Kidedea'
Mapambano haya yoteyatafanyika siku hiyo katika ulingo mpya wa mdau wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego' aliejenga ulingo uho kwa ajili ya kuwakombowa mabondia na hadha ya kupigania chini
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katikamchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani