Quantcast
Channel: MZUKA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Article 9

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Dkt. Kolimba kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Desemba 31, 2015




Mhe. Balozi Al Najib akimkabidhi Mhe. Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait




Sehemu ya ujumbe kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Kolimba na Balozi wa Kuwait hapa nchini (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Batholomeo Jungu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Tahir Bakari, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri.



Picha ya pamoja


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na  Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat. Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Desemba, 30, 2015.

 Waziri akipozi kwa picha na mgeni wake
 Waziri katika mazungumzo na mgeni wake



Balozi Mteule Mhe. Shabat akimkabidhi Mhe. Mahiga zawadi ya picha inayoonesha Kanisa  lililopo katika mji wa  Jerusalem

 Picha ya pamoja


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Qatar Mhe. Abdullah Jassim Almaadadi alipofika Wizarani kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa katika wadhifa wake mpya na pia kumhakikishia ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 30 Desemba, 2015.

 Waziri akizungumzana mgeni wake
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kulia, akimkaribisha ofisinikwake, Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, alipokuja kumtembelea Wizarani na kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait na pia kumpongeza.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, alipokuja kumtembelea Wizarani na kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait na pia kumpongeza.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1239

Trending Articles