Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kikanda katika viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.
Afisa wa SSRA, Bi. Aminah Kisisa akigawa vipeperushi kwa moja ya wadau waliotembelea Banda la SSRA kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Afisa wa Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA Bw, Ally Masaninga akifafanua kwa mmoja ya wadau waliotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Timu ya SSRA katika picha ya pamoja wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.
Sehemu ya wafanyakazi wa SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi Sarah Kibonde Msika, akimkabidhi mfuko wa SSRA pamoja na Vipeperushi Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati Bw, Mwinuka, Maonesho hayo yanaendelea Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika akiwa na wadau waliotembelea Banda la SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.